NEYMAR AFUNGUA MICHUANO YA MABARA KWA GOLI KALI

Hapo jana (Juni 15,2013) Usiku kwenye mchezo wa Ufunguzi wa Kombe la MABARA ,Wenyeji Brazil walianza kwa kishindo Mechi yao ya KUNDI A iliyochezwa uwanja wa Estadio Nacional de Brasilia Mjini Brasilia kwa kuwatandika Mabingwa wa Asia Japan Bao 3-0.


Bao za Brazil zilifungwa na Neymar, kwa Bao safi sana la Dakika ya 3 tu, na Paulinho kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 48 na Jo kufunga la mwisho katika Dakika za Majeruhi.


Leo (JUNI 16,2013) Usiku zipo Mechi mbili kati ya Mexico v Italy, KUNDI A kasha kufuatiwa na Mechi ya KUNDI B kati ya Mabingwa wa Dunia Spain v Uruguay.

Comments