
Baada ya wapenzi wa muziki Tanzania
kusubiri kwa muda mrefu sasa wamepata nafasi ya kujiburudisha na ngoma
mpya kutoka kwa Alikiba. Tarehe 25 Julai, 2014 Alikiba ameachia single
mbili mpya kwa wakati mmoja ziitwazo “Mwana” na “Kimasomaso”. Alikiba
anajulikana ndani na nje ya Tanzania kwa hit zake kama Cinderella,
Mapenzi yanarun dunia, Single boy, na Dushelele. Cinderela ndiyo wimbo
ambao mpaka sasa umeweka rekodi ya kuuza copy nyingi katika Afrika
Mashariki mwaka 2008. Mwaka 2012 Alikiba alishinda tuzo ya best Rhumba/
Zouk na wimbo wake wa “Dushelele” katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania
Music Awards. Alikiba anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kuimba na
utunzi wa nyimbo pamoja na kuwa mburudishaji mkali sana katika show zake
za live na mpaka sasa ametembea nchi nyingi sana duniani kuburudisha
wapenzi wa muziki. Sasa unaweza kupata nyimbo mbili mpya za Alikiba
katika tovuti ya www.mkito.com
Kimasomaso – https://mkito.com/song/kimasomaso/2194
Comments
Post a Comment