Kucha wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini kuwa Chelsea ndiyo klabu inayotegemewa kushinda taji la ligi msimu huu lakini anasisitiza kuwa timu yake iko tayari kupambana kwa taji kupitia njia zote.
Arsenal ilishinda Kombe la FA kwa mwaka wa pili mfululizo msimu uliopita lakini ilishika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Uingereza, ikiwa na alama 12 nyuma ya mabingwa Chelsea.
Na kusajiliwa kwa kipa Petr Cech kutoka wapinzani wao wa London Chelsea yaweza kuwafanya wawe wapinzani wakubwa kwa kombe.
"Chelsea ilishinda kombe kwa kiasi mwaka jana kwa hiyo ni lazima washinde tena,'' aliwaambia watangazaji habari.
"Tuko tayari kupigania ubingwa. Tulikosea mwanzo wetu wa msimu mwaka jana, hebu tujaribu kuanza na nguvu. Lakini tunakuwa na mwanzo usio rahisi kwa uhasimu wa timu mbili na Liverpool katika mechi zetu tatu za kwanza.
"Sisi hufurahia [shinikizo la kusema kama washindi]. Kabla, hakuna mtu aliyekuwa akitusema kama vile! Tulipita kipindi hicho."
Arsenal itaikaribisha West Ham katika Emirates Jumapili hii mchana katika mechi yao ya ufunguzi wa kampeni ya Ligi Kuu.
Comments
Post a Comment