Katika mchezo huo mkali ambao ulimalizika dk 90 kwa magoli manne kwa manne kwa Timu zote mbili.Sevilla walipata bao la kuongoza kutoka kwa mchezaji wao Ever banega dakika za mwanzoni kabisa dk ya 3 na barcelona kujibu mapigo kutoka kwa mshambuliaji wao Lionel Messi Ambaye amepachika magoli mawili katika mchezo huo dk ya 7 na ya 16 Huku mchezaji wa barcelona Rafinha akipachika bao la 3 kwenye dakika ya 44 na timu zikienda mapumziko barca 3 sevilla 1
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kushambuliana huku Suarez akipachika msumali wa nne kwa barca dakika ya 52.Kunako dakika ya 57 Jose Antonio Reyes aliwapatia Sevilla goli la pili na dk ya 72 Kevin Gameiro aliwapatia goli la tatu kwa mkwaju wa penati mpaka dakika ya 81 Yevheniy Konoplyanka alipachika goli ka nne kwa Sevilla na kufanya mchezo huo kuwa droo na kuenda Extra time.
Kwenye dakika ya 93 Mchezaji anayewaniwa na Manchester UTD pamoja n Manchester city Pedro Rodriguez anaingia akitokea benchi na kuipa bao la ushindi barca kwenye dk ya 115 na kufanya matokeo yawe Barcelona 5 - 4 Sevilla
Comments
Post a Comment