HEKIMA ZA MASSAWE
Nashukuru mwenyezi mungu kwa kunipa afya njema ..natumai ni kwa mara ya kwanza ninawaletea hekima zangu kwenu..
Leo nitagusa maswala ya kisiasa kwa uchache zaidi ni matumaini yangu mtanielewa kile nachotaka kufikisha kwenu.
Miaka miwili nyuma nilisoma kitabu kimoja cha moja ya aliekuwa senetor wa marekani aitwaye .."Gavin de becker" kitabu chake kinaitwa "gift of fear" labda ni kwanini nkiongelea kitabu hichi..
Hivi majuzi nikiwa katika mtaa mmoja hapa mjini katika mihangaiko yangu nilikutana na kikundi kimoja kikiwa kina ingelea maswala ya kisiasa lakini katika kikundi hiki walikuwa wakibishana kishabiki zaidi na hata kunifanya nisimamishe shughuli zangu na kufuatilia ubishi ule uliokuwa wakusisimua kweli kweli..kulikuwa na upande wa chama tawala na upande wa mungano wa ivi vyama vya upinzani.. mmoja ya watu walikuwa wakichangia pale alikashifu mwenzake akidai chama chake ni cha (kikabila,udini) nilipatwa na hofu hasa nikijua kulikuwa na watu tofauti maeneo yale .. ila nilijiwa na kumbukumbu zikiniambia hawa wana siasa ndio wametufikisha hapa ....Hasa ukizingatia ndio hao wanaobishana majukwaani na kuchafuana kwa hizi propaganda na hapa ndipo nikakumbuka maneno ya gavin de becker "
Every human behavior can be explained by what precedes it,but that does not excuse it "hakiwa na maana kila tabia ya binadamu inaweza kuelezwa kwa lile lililopita lakini lisiwe dhuru.. Ni kwa nini nasema ivi ni kwasababu ya kile tunachokishuhudia kwenye siasa wakati huu.. vyama vinatumia nguvu nyingi kwenye propaganda pasipo kutengeneza muundo mzuri wa kueleza ni jinsi gani watatatua matatizo yetu...vipao mbele vimekuwa ni udini,ukabila pasipo kuangalia mambo muhimu na mustakabali wa taifa hili.. binadamu tumetofautina sana mana wapo wanaopiga kura kwa kufuata propaganda bila ya kujua utofauti wa propaganda na sera..mwananchi wa taifa hili unapaswa kuangalia,kusikiliza,kusoma na kuelewa kua siasa inamsaada gani kwako katika kumteua mtu sahihi nasikitika elimu hii haipo kwetu sisi na ndio manaa..Tunaambiwa tukichagua chama fulani nchii hii itaingia kwenye maasi,vita na machafuko na hili tumelisikia jukwaani! Je ebu niambia unamjengaje huyu mwanachi kwa haya maneno?......labda tu gavin de becker alinipa maneno sahihi juu ya hili nayo ni
"The solution to violence in Tanzania is the acceptance of reality" Na hii ndio njia sahihi je unaye sema maneno hayo unakubali uhalisia? Tujaribu kusikiliza na kujenga hoja za msingi kwa taifa letu na si kujitengenezea uhadui .... imeandaliwa nami (daniel faustine)
Comments
Post a Comment